Saluti Dogo!! Mshambuliaji Didier
Drogba wa Galatasaray, akimpa mkono wa pongezi mchezaji mwenzake
Emmanuel Eboue baada ya kufunga bao la kusawazisha dhidi ya Real Madrid,
katika mechi ya marudiano ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya
iliyoisha kwa Galatasaray kushinda 3-2. Hata hivyo Madrid ilisonga kwa
ushindi wa jumla wa mabao 5-3. (Picha zote kwa hisani ya gazeti la Daily Mail la Uingereza)
Kisigino cha Dhahabu Hicho: Drogba
akipiga kisigino na kufunga bao katika mechi hiyo kwenye dimba la Turk
Telecom Arena jijini Istanbul, Uturuki.
I am that I am: Drogba akishangilia baada ya kufunga bao.
Mama Yanguuuu!!!! Cristiano Ronaldo na
Gonzalo Higuain wa Madrid, wakisikitika baada ya timu yao kukubali
kufungwa mabao mawili ya haraka haraka ndani ya dakika tatu.
Kitu Kambani Kudadadeki: Wesley Sneijder wa Galatasaray, akikimbia kushangilia bao lake dhidi ya Madrid.
No One Like Me!! Ronaldo akishangilia bao la kwanza katika mechi hiyo ambayo aliifungia Madrid mabao yote.
Never Give Up Guys: Wachezaji wa Madrid
wakihamasishana baada ya kuruhusu mabao mawili ndani ya muda wa dakika
tatu, huku Drogba kulia akisali kumshukuru Mungu kwa kumuwezesha
kufunga.
GOD is Good: Ronaldo akionesha kidole
kimoja juu, kama ishara ya kumshukuru Mungu aliyewawezesha kusonga mbele
hata baada ya kufungwa mechi yao na Galatasaray.
Kiona Mbali: Mashambiki wa Borussia
Dortmund, wakionesha tambala la kibonzo chenye darubini kuangalia mbele
waendako, na hii ni kabla ya kuanza kwa mechi iliyoisha kwa kuibuka na
ushindi usiotarajiwa wa mabao 3-2 dhidi ya Malaga kwenye dimba la Signal
Iduna Park, Dortmund Ujerumani.
I am Brazilian: Santana (27)
akishangilia na wachezaji wa Dortmund baada ya kuibuka na ushindi wao,
uliokuja baada ya mabao mawili yaliyofungwa katika dakika tatu za
nyongeza (likiwamo lake yeye la ushindi) na kutinga nusu fainali ya
mabingwa Ulaya.
Tumetishaaaaaaaaaa!!! Wachezaji na viongozi wa Dortmund wakishangilia ushindi huo.
Huwezi Kuzuia Mvua Wewe!!! Joquin
Sanchez wa Malaga (kulia), akifumua shuti kuifungia timu yake bao la
kwanza dhidi ya Dortmund, huku jitihada za kuzuia za beki wa Dortmund
zikishindwa kuzaa matunda.
Back in the Net: Joquin Sanchez akishangilia bao hilo, huku nyota wa Dortmund wakiwa hawaamini macho yao kama wanavyoonekana.
Hureeeee!!!! Wachezaji wa Malaga wakimpongeza Joquin Sanchez.
Ferguson Ananipendea Hiki: Robert Lewandowski akimtambuka mlinda mlango wa Malaga na kuifungia Dortmund bao la kusawazisha.
No One Like Me!!! Robert Lewandowski akishangilia baada ya kuifungia Dortmund bao la kusawazisha.
Kama Kumsukuma Mlevi: Santana
akiifungia Dortmund bao la ushindi kilaiiini mwishoni mwa mechi hiyo na
kuiwezesha kufuzu nusu fainali Ulaya.
No One Like You Santana: Kocha wa Dortmund Jurgen Klopp, akiruka juu kushangilia bao la ushindi wa kikosi chake lililofungwa na Santana
Haikuwa Kazi Rahisi: Wachezaji wa Dortmund wakishangilia kufuzu nusu fainali baada ya kuing'oa Malaga.
No comments:
Post a Comment