Waimbaji wa Nyimbo za Injili katika amasha la Pasaka linalo
andaliwa na Msama Promotion, wamezidi
kuingia jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Kutumbuiza kwenye Tamasha hilo
litakalofanyika siku ya Jumapili katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Miongoni mwa Wasanii walioingia jijini Dar kwa ajili ya
Tamasha hilo ni pamoja na Solomon Mukubwa kutoka Nchini Kenya, pamoja na Msanii
Faraja Kutoka Nchini Kongo ambapo wameahidi kushusha Upako siku ya Tamasha hilo
na hivyo wamewataka Watanzania wajitokeze kwa wingi kwenye Tamasha hilo.
Solomon Mukubwa amesema kuwa, ana ahidi watu kuona Uwepo wa
Mungu siku hiyo kwani anaamini kabisa
kuwa Mungu amewapa Watanzania Amani kwahivyo kwa kupitia Wimbo wake wa Mfalme
wa Amani Kila mtanzania atakayekuwepo siku hiyo ataondoka na Amani.
Aidha
Mkurugenzi wa Msama Promotions ambao ni waandaaji wa tamasha hilo, Alex Msama
amesema kuwa Msanii Sipho Mwakaba kutoka Afrika ya Kusini anatarajiwa kuingia jijini Dar es Salaam siku ya Ijumaa na kuongeza kuwa siku ya Tamasha utafanyika uzinduzi wa albam ya kundi la Gloria
Celebrations ‘Kwetu Pazuri’ itakayojulikana kama ‘Kuweni Macho’ ambayo itauzwa
siku hiyo.
Tamasha hilo ambalo
litafanyika pia katika mikoa ya Mbeya Aprili Mosi, Iringa Aprili 3, Aprili 6
mkoani Dodoma na Mwanza Aprili 7.
Viingilio katika tamasha hilo kwa VIP ni shilingi 50,000, Viti maalum shilingi 10,000, Viti vya kawaida 5000 na watoto shilingi 2000.
Mgeni rasmi katika tamasha
hilo ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
No comments:
Post a Comment