Daladala likipita kwa tabu katika barabara ya Azikiwe Posta jijini Dar es Salaam leo.
Mtaa wa Azikiwe ukiwa umefurika maji ya mvua.
Adha ya mvua gari likiwa limetumbukia katika chemba ya maji machafu.
Wasamaria wema wakisukuma gari la polisi lenye
namba PT 0314 baada ya kuzimika barabarani kufuatia mvua kubwa iliyonyesha
katika maeneo ya katikati ya jijini Dar es Salaam
Mvua kubwa iliyonyesha katika maeneo mbalimbali ya jiji la
Dar es salaam leo, ilisababisha adha kubwa kwa watumiaji wa barabara, kutokana
na nyingi kati ya hizo kushindwa kupitika kwa urahisi baada ya kujaa maji kama
picha inavyoonesha gari lenye namba za usajili T 339 CGJ likipita kwa tabu katika
barabara ya Azikiwe, katikati ya jiji.
Wakazi
wa Tabata Kisiwani wakivuka mkondo wa maji kufuatia mvua kubwa iliyonyesha katika
maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam leo na kusababisha mafuriko.
Habari
zilizotufikiwa katika chumba chetu cha habari zinasema kuwa mvua kubwa
iliyoanza majira ya saa nne asubuhi imesababisha maafa baada ya mtu
mmoja kuzolea na maji ya mvua katika eneo la Tabata Reli jijini Dar es
Salaam.
No comments:
Post a Comment