Monday, March 25, 2013

JUKWAA LA KATIBA TANZANIA YAITAKA TUME YA KATIBA KUSHIRIKISHA WANANCHI KATIKA SWALA ZIMA LA MCHAKATO WA UTAFUTAJI WA MAONI YA KATIBA MPYA


Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania Bw, Deus Kibamba (aliyvalia Shati jekundu) akifafanua Jambo Mbele ya Waandishi wa Habari leo katika Makao Makuu ya Ofisi ya Jukwaa la Katiba jijini Dar es Salaam ambapo amezungumzia Mchakato wa Kura za maoni juu ya Rasimu ya Katiba Mpya Zimbabwe na Mafunzo Makuu kwa Mchakato wa katibba Mpya Tanzania.
Amesema kuwa Moja ya Sababu iliyosababisha Zimbabwe kukosa Katiba yenye uhakika ni kukosekana kwa Elimu ya Uraia kwa Wananchi pamoja na kutoshirikishwa kwa Wananchi katika Swala zima la Mchakato wa kutafuta Maoni.


 Bw Kibamba amesema kuwa, yanahitajika Marekebisho ya Haraka ya Sheria ya Mabadiliko ya katiba ya Mwaka 2011 ili kuboresha Bunge la katiba na kura ya Maoni ikiwemo kuweka tarehe Muhimu za Matukio.

"Marekebisho hayo yalikwisha andikwa na  Mhe, Rais Dk Jakaya Mrisho Kikwete na itakuwa ni kumwangusha endapo hayatatekelezwa", amesema Kibamba.

Amesema kuwa, Mabadiliko yanayohusu muundo na Uteuzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Sheria Zote zinazohusu uchaguzi yafanyike sasa ili kuondoa hofu iliyopo Nchini kuwa tume hii inatumika  kubadilisha matokeo au kuchakachua kama inavyojulikana mitaani.

Ameongeza kuwa, Wananchi wanapaswa kushirikishwa katika mchakato mzima hadi kupatikana kwa katiba mpya, kwani wasiposhirikishwa watakata tamaa na kuacha mchakato mzima kubaki kuwa ni wanasiasa pekee, ambapo jambo hilo linapelekea kuwepo kwa mwitikio mdogo sana katika mchakato mzima wa wa kura ya maoni ya katiba mpya.

Aidha ameongeza kuwa, kutokana na uchaguzi wa Zimbabwe Tanzania inapaswa kujifunza kuwa, kuchelewa kwa fedha kwa ajili ya kura za Maoni, ambapo Zimbabwe walipata fedha za kuendeshea shughuli nzima za kura ya Maoni siku chache kabla ya zoezi la kupiga kura ya maoni ambapo fedha nyingi zilipatikana kwa kuchelewa, ambapo Tanzania inajifunza kuwa  maandalizi ni jambo la Msingi yaani upatikanaji wa Fedha za uhakika mapema.
 

Mdau kutoka katika Ofisi ya Jukwaa La Katiba akichukua Matukio katika mkutano huo

Meza kuu katika Mkutano huo.

No comments:

Post a Comment