Friday, February 8, 2013

Rais Kikwete azindua utoaji wa Vitambulisho vya taifa katika viwanja vya Karimjee leo


8E9U6208Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akibonyeza kitufe kuashiaria kuzindua rasmi mfumo wa usajili na utambuzi wa watu na utoaji wa vitambulisho vya taifa uliofnyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.Watatu kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Dkt.Emmanuel Nchimbi, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Bwana Mwaimu na kulia nia Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Bwan Said Meck Sadik.
(Picha na Freddy Maro)
8E9U6279Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiangalia bango lenye kitambulisho cha  taifa cha Rais Kikwete muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuzindua mfumo wa Usajili na utambuzi wa watu na utoaji wa vitambulisho vya taifa uliofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Waziri wa Mambo ya  Ndani ya Nchi Dkt.Emmanuel Nchimbi.
8E9U6352Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt.Emmanuel Nchimbi akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kitambukisho cha Taifa katika hafla ilkiyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
8E9U6396Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rais Mstaafu awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi kitambulisho chake cha taifa katika viwanja vya Karimjee leo.
8E9U6404Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa kitambulkisho cha taifa katika viwanja vya Karimjee leo.
8E9U6416Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rais Mstaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume kitambulisho chake cha taifa katika viwanja vya Karimjee leo.
8E9U6428Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad kitambilisho cha Taifa katika viwanja vya Karimjee leo wakati wa hafla ya Uzinduzi wa mfumo wa usajili na utambuzi wa watu.

No comments:

Post a Comment