Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema (kulia),
akihutubia katika sherehe za mahafali ya 19 ya Kidato
cha sita katika Shule ya Sekondari ya Jitegemee Mgulani
JKT Dar es Salaam leo asubuhi. Wengine ni
walimu na wafanyakazi wa shule hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema, amewataka walimu wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee kuandika barua ya maombi kwa Manispaa ya wilaya hiyo ili wapate viwanja vya kujenga nyumba zao kama motisha ya serikali kwao.
Mwito huo ulitolewa na Mkuu huyo wa wilaya ya Temeke wakati akizungumza na walimu hao baada ya kumalizika kwa mahafali ya 19 ya kidato cha sita ya shule hiyo Dar es Salaam leo ambapo alikuwa ni mgeni rasmi.
"Serikali inajua mazingira magumu mliyonayo hasa ninyi walimu muliopo mjini kwani hamna njia nyingine ya kujiongezea kipato" alisema Mjema.
Alisema walimu waliopo vijijini wanafursa kubwa ya kupata motisha ya kupewa mashamba na kulima hivyo kujikomboa kiuchumi tofauti na wale wa mjini.
"Nitawasaidieni katika maeneo mawili kwanza ninyi kama taasisi andike barua kuomba maombi ya kupata ardhi kwa ajili ya kufanyia shughuli zenu mbalimbali na mimi nitasaidia kulifanyia kazi jambo hilo" alisema Mjema.
Alisema katika eneo la pili kwa kila mwalimu aandike maombi ya kuomba kiwanja kwani vipo maeneo ya Kimbiji ambapo kiwanja kimoja kinauzwa sh.8,000 kwa mita moja.
Aliwataka walimu hao kuchangamkia fursa hiyo haraka iwezekanavyo wakati akiwa bado yupo katika wilaya hiyo kabla Rais Jakaya Kikwete haja muhamishia wilaya nyingine.
"Ningependa kuona nawasaidieni katika jambo hili kabla sijaondoka katika wilaya ya Temeke naamini mkiwa na mazingira mazuri ya kuishi mtatoa elimu bora kwa watoto wetu" alisema Mjema.
Alisema kwamba viwanja hivyo
vikipatikana na kuwa na hati miliki itasaidia kuwa dhamana ya kupata
mikopo kutoka katika taasisi za fedha.
Mkuu wa Shule hiyo Luteni Kanali Martin Mkisi alitumia fursa hiyo kumshukuru mkuu huyo wa wilaya kwa kuonesha nia ya kuwasaidia walimu wa shule hiyo na kwamba mchakato huo utafanyika haraka.
Mkuu wa Shule hiyo Luteni Kanali Martin Mkisi alitumia fursa hiyo kumshukuru mkuu huyo wa wilaya kwa kuonesha nia ya kuwasaidia walimu wa shule hiyo na kwamba mchakato huo utafanyika haraka.
No comments:
Post a Comment