Wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha cha jijini Dar es Salaam (IFM)
wameandamana leo majira ya adhuhuri hadi kwenye Wizara ya Mambo ya
Ndani wakiwa na madai ya kutopewa ulinzi na jeshi la polisi kwenye
makazi yao ya hosteli za Kigamboni kutokana na kuvamiwa na majambazi
mara kwa mara.
Wanafunzi hao walidai
kuwam, siku ya Ijumaa walifanya kikao na jeshi hilo ili wawape ulinzi
lakini suala la ajabu ni kuwa, siku waliyofanya kikao na Jeshi hilo
ndiyo siku wenzao wawili wakiume walipovamiwa na kulawitiwa.
Majambazi hao wamekua wakidai wapewe laptops, simu na fedha na kama mwanafunzi anakataa, humlawiti.
Rais
wa Serikali ya wanafunzi ya Chuo cha IFM alizungumza leo na Kamanda wa
Polisi wa Kanda maalumu ya Kipolisi ya jiji la Dar es Salaam Suleiman
Kova mara baada ya kuwasili eneo la ofisi za Wizara ya Mambo ya ndani
ambapo amesema, "Wanafunzi wenzetu wa kiume wamelawitiwa nyinyi tumewapa
taarifa siku ya ijumaa kuwa hatunaulinzi tunaibiwa hovyo vitu vyetu
halafu siku hiyo hiyo unafanyika ubakaji huo…" ndipo kamanda Kova
aliwaamuru wanafunzi hao wafuatane naye waende hadi Kigamboni kwenye
Kituo waliporipoti taarifa zao pamoja na kwenda kwenye Hosteli zao. Kova
aliahidi kushughulikia jambo hilo kwa haraka bila kusita.
------------------------------------------------------------------
|
Walifika Wizara ya Mambo ya Ndani |
|
Tupo kamili fanyeni Fujo muone |
|
Rais
wa Serikali ya Wanafunzi IFM akimweleza Kamanda wa kanda Maalum ya Dar
es Salaam Suleiman Kova juu ya Malalamiko ya wanafunzi wenzake. |
|
Umati wa wanafunzi wa IFM |
|
Kamanda
wa Kanda maalumu ya Dar es Salaam akizungumza na wanafunzi wa IFM
kuhusiana na maandamano yao ambapo aliwataka waongozane wote mpaka
Kigamboni kwenye vyumba vyao. |
|
Wakiwa kwenye Safari ya kuelekea Kigamboni Kumpeleka Kamanda Kova wakitokea Wizara ya Mambo ya ndani |
|
Bado safari inaendelea hapa wakiwa kwenye Kivuko cha kuelekea Kigamboni |
No comments:
Post a Comment