Kamanda wa mkoa wa kipolisi wa Kinondoni Charles Kenyela akizungumza na waandishi wa habari leo katika makao makuu ya jeshi la polisi Mkoa wa Kinondoni |
Akiszungumza na waandishi wa Habari kamanda Kenyela amesema kuwa tukio hilo limetokea tarehe 09/01/2013 maeneo ya Kimara Bonyokwa kwenye nyumba ya Mtu aliyefahamika kwa Jina la Issa Omary mwenye umri wa miaka 39.
Kamanda Kenyela amesema kuwa wamewakuta watuhumiwa hao wakiwa wamefungiwa kwenye Chumba kimoja ndani ya nyumba ya Omary na walibaini kuwa watuhumiwa hao wametokea Nchini Ethiopia na wengine wametoka Burundi ambapo wangesafirishwa kwenda Afrika ya Kusini kupitia Mpaka wa Mtwara.
Ameendelea kusema kuwa, wahamihaji hao hawana hawakuwa na hati ya kusafiria isipokuwa huvushwa mpaka hadi Mpaka na watu maalum walioandaliwa na wasafirishaji(Traffickers)
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Ndayeshimeye Abdulkabir (30) Mrundi mkazi wa Msava Kayanzi ambaye ni Mfanya Bihashara pamoja na Nduwayezi Blaise (24) Mrundi mkazi wa Bujumbura mwanafunzi wa Chuo cha Bridge College ambao hao ndio wahusika wakuu wa Usafirishaji wa wahamiaji haramu wanaotokea Ethiopia.
Hawa ndio wafanya Bihashara wakuu wa kusafirisha Binadamu Ndayeshimye pamoja na Mwenzie Nduwayezi wakiwa chini ya ulinzi |
Watuhumiwa 7 wakiwa chini ya Ulinzi |
Huyu ndiye Omary, Mtanzania aliyewahifadhi wahamiaji Haramu |
Kamanda Kenyela akisema Machache na Wafanya Bihashara ya Usafirishaji Binadamu |
No comments:
Post a Comment