![]() |
(PICHA ZOTE KWA HISANI JUMA MTANDA BLOGSPOT
|
Sehemu ya vijana wakiwa katika picha
tatu tofauti mara baada ya kuchoma moto na kufunga barabara barabara
kuu ya Dodoma-Morogoro kwa kuweka vizuwizi mbalimbali hali iliyopelekea
watumia wa barabara hiyo kushindwa kuitumia kwa masaa matano kabla ya
polisi kutuliza hali hiyo iliyoanza majira ya saa 2 asubuhi na kudumu
hadi majira ya saa 7 mchana katika mji mdogo wa Dumila wilaya ya Kilosa
mkoani Morogoro.

Vijana wakazi wa Dumila na vitongo vyake
wakiangusha gari aina ya Land Cruizer T 241 AMS mali ya mfugaji katika barabara
kuu ya Dodoma-Morogoro wakati wa vurugu zilizodumu kwa masaa sita kwa kuweka vizuwizi
kwa lengo la kumshinikiza mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bebdera kusikiliza kero
za wakulima.
Askari wa kutuliza ghasia (FFU) Morogoro wakiangalia gari mara baada ya kuharibiwa wakati wa vurugu hizo kabla ya kulinyanyua.
Gari hili likionekana mara baada ya
kuharibiwa likiwa katikati ya barabara kabla ya kusukumwa na kulirejesha
sehemu ambayo iliegeshwa.
Mwananchi akizngumza jambo na askari wa
kutuliza ghasia muda mfupi kabla ya mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera
kuhutubia wananchi hao na amani kurejea katika hali yake ya kawaida.
Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Morogoro
(RCO), Hamisi Selemani (kushoto) akiawaangalia vijana waliokuwa wakiimba
nyimbo mbalimbali wakati wakimsubiri mkuu wa mkoa wa Morogoro ili
awahutubie.
Rasta Man kushoto akijaribu kuwatuliza wananchi wenzake kabla ya mkuu wa mkoa wa Morogoro kuhutubia. 

Sehemu ya akinamama wakionyesha kukerwa
na jambo wakati wa vurugu hizo, hapa walikuwa wakimsubiri mkuu wa mkoa
wa Morogoro ili kuweza kusikiliza kero zao. 

Mmoja wa vijana akitoweka na kreti la chupa tupu za soda mara baada ya kupora katika vurugu hizo.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel
Bendera akiwahutubia umati wa wananchi wa vijijini vyenye migogoro ya
ardhi katika tarafa ya Magole wilaya ya Kilosa kwenye uwanja wa shule ya
msingi Dumila jana.
Gari la mkoa wa Morogoro likiondoa eneo la mkutano wa hadhara
uliofanyika katika eneo la shule ya msingi Dumila wilaya ya Kilosa
mkoani hapa.
VURUGU TUPU MIKOA YA MOROGORO, DAR ES SALAAM NA MTWARA.
Mmoja afariki Dumila, wengine wajeruhiwa, nyumba ya Ghasia yavunjwa Mtwara.
Kwa ufupi.
Mkoani Mororgoro mtu mmoja
aliyefahamiwa kwa jina la Mohamed Msigara (60) amefariki dunia na wengine
kadhaa kujeruhiwa baada ya kutokea vurugu kati ya wakulima na wafugaji Kijiji
cha Dumila, wilayani Kilosa, baada ya wafugaji wa Jamii ya Kimasai kuingiza
mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima yaliyo katika Kitongoji cha Mfulu,
Kilosa.
No comments:
Post a Comment