Rais Barack Obama akila kiapo cha kuiongoza nchi ya Marekani muhula wa pili mbele ya familia yake.

Makamu wa rais wa Marekani Joe Biden naye akifanya vivyo hivyo.
Rais Barack Obama wa Marekani ameapishwa kwa ajili ya muhula wake wa pili katika hafla iliyohudhuriwa na wanafamilia na waandishi wa habari pekee.
Rais Obama anaanza muhula wa pili akikabiliwa na matatizo kadhaa nyumbani na nje, yakiwemo mgawanyiko mkubwa mjini Washington kuhusu masuala mbalimbali, mpango wa Iran wa nyuklia na wapiganaji wa Kiislamu katika kanda ya Afrika ya kaskazini.
Sherehe kubwa inatarajiwa kufanyika leo katika jengo la Capitol mjini Washington, ambapo hotuba ya Obama inatarajiwa kujikita katika haja ya kufanya tahfif za kisiasa na warepublican pale inapowezekana.