Tuesday, January 22, 2013

MTOTO AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA MOTO MBEYA

Mwili wa mtoto huyo ukichukuliwa na polisi kwenda kuhifahiwa na kuchunguza chanzo cha moto huo
Nyumba hii ndimo alimoungulia mtoto huyo
Baadhi ya majirani wakiwa katika tukio hilo 

 Mtoto Halaika Bushiri (7) mwanafunzi wa shule ya msingi Mwanyanje iliyopo kata ya Igawilo Mkoani Mbeya amefariki dunia baada ya kutekea kwa moto akiwa nyumbani kwao jana majira ya saa 7:45 ya mchana, Januari 21 mwaka huu.
  

Shuhuda wa tukio hilo Recho Jeseph (36) amesema mtoto huyo aliaza kupiga kelele za kuomba msaada mara baada ya kutokea kwa moto wakati mama wa mtoto Nuru Mlele akiendelea na  shughuli zake licha ya majirani, kujitokeza na kuuzima moto huo.
  
Katika hali ya kushangaza mama huyo hakuonesha kustushwa na kitu chochote na wakati tukio hilo aliendelea kufua nguo, hadi pale majirani walipofanikiwa kuudhibiti moto huo ambao uliteketeza samani za nyumba yake ikiwemo seti moja ya kochi.


Aidha kutokana na juhudi za majirani kushirikiana ndani ya dakika kumi walifanikiwa kuudhibiti moto huo na kuuzima lakini mtoto huyo alikuwa tayari ameshafariki.

Hata hivyo licha ya polisi kupewa taarifa majira ya saa tisa kamili walifika majira ya saa kumi na mbili na robo jioni, eneo la tukio lenye umbali wa mita mia sita kutoka kituoni, hali iliyowasononesha wananchi wengi.

  
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amekiri kupokea taarifa za tukio hilo na kuongeza kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa na uchunguzi zaidi wa tukio hilo bado unaendelea.

Na Ezekiel Kamanga,Mbeya

No comments:

Post a Comment