Sunday, January 27, 2013

MGOGORO KANISANI WASABABISHA IBADA ISIFANYIKE,,, KISA WANAGOMEA KANISA

Kipeperushi kikiwa kimebandikwa kwenye mlango wa kanisa kinacho onyesha kutokuwepo kwa Ibada leo katika kanisa la Moravian Usharika wa Tabata jimbo la Mashariki na mlango ulikuwa umefungwa waumini wasiweze kuingia kanisani kufanya Ibada.
 Migogoro ya Kidini imeendelea kushika nafasi hapa Tanzania, hii imetokea tena leo jijini Dar es Salaam baada ya Baraza la wazee kufunga mlango wa kanisa la Moravian kutokana na kutoelewana baina ya pande mbili kati ya viongozi wa chini ambao ndio Baraza la wazee na Viongozi wa juu wa kanisa hilo wakiwemo Mwenyekiti wa Kanisa hilo.

Ugomvi katika kanisa hilo umesababishwa na umiliki wa kanisa ikiwa wazee wanadai kanisa ni lao na viongozi wa juu wanadai kanisa ni lao na tayari wana vielelezo vyote vya kuruhusiwa kumiliki kanisa hilo.

Akizungumza katika mgogoro huo Mwenyekiti wa kanisa hilo Mch, Clement Mwakibete amesema kuwa yeye anavielelezo vyote vinavyo mfanya awe anamiliki kanisa hilo.


Wachungaji viongozi wa kanisa hilo wakiwa nje ya wamekaa baada ya mlango wa kanisa kufungwa na wazee wa Baraza,

Viongozi wa kanisa hilo wakijadiliana Jambo na waandishi wa habari

Waumini waliendelea kufanya Ibada nje ya kanisa hapa waki imba nyimbo za kusifu

Baada ya Muda kidogo Kamanda wa polisi wilaya ya Ilala Bi Marietha Minagi aliwasili eneo hilo na akajadiliana na Viongozi wa kanisa kuwa Ibada isifanyike  mpaka watakapo kwenda kuonana na Waziri wa mambo ya Ndani hapo kesho kwa ajili ya Kutafuta Suluhu hata hivyo Mweneyekiti wa kanisa hilo alisema hata hudhuria kwa Waziri kwani Vielelezo vyote anavyo na amepewa na serikali.

Hawa ndio viongozi wa kanisa hilo hapa wakimsikiliza kamanda kwa Makini
Kanisa lenyewe ndio hili

Mchungaji Clement akionyesha hati za Umiliki wa kanisa hilo

Huyu ni ni Mmoja wa Wazee waliofunga kanisa ambaye hakutaja jina lake na hakuzungumza chochote kwa kisingizio kuwa yeye siyo msemaji.

No comments:

Post a Comment