MAMLAKA ya Mawasiliano nchini
(TCRA), imewatoa hofu wananchi wote wanaoishi katika maeneo ambayo mfumo
mpya wa mawasiliano Digitali haujafika kuwa wataendelea kupata
mawasiliano kupitia mfumo wao wa zamani Analojia.
Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar
es Salaam jana, na Meneja wa Mawasiliano wa Mamlaka hiyo, Inocent Mungi,
kuhusu wasiwasi uliyojitokeza kwa wananchi haswa waliyoko mikoani.
Mungi alisema watazima mtambo
wazamani kule ambako huduma ya hiyo mpya ya Digitali imefika, hata
hivyo, kwenye maeneo ambayo hayajafikiwa na mtambo huo mpya, yataendelea
kutumia Televisheni zao kupitia mfumo wazamani.
Alibainisha kuwa hadi sasa ni
asilimia 24 sawa na mikoa 11 ya nchi ndiyo itafaidika na mawasiliano
hayo ya Digitali, ambapo kule kusiko kuwa na mawasiliano hayo bado
wataendelea kupata mawasiliano kwa kutumia Setelait, madishi na
usambazaji wa nyaya hadi hapo mfumo mpya utakapo wafikia.
“Naomba niwatowe hofu wananchi
kuwa siyo kweli kwamba ifikapo Decemba 31, serikali itazima nchi nzima
mtambo huo wa Analojia, hiyo haiwzekani na wala siyo rahisi kufikisha
huduma ya Digitali kwa mara moja katika maeneo yote ya nchi”alisema
Mungi.
Aidha, alitoa wito kwa wananchi
kuwa wasikubali kudanyika na maneno ya mitaani kuwa Televisheni za
kichogo mara ifikapo mwishoni mwa mwezi huu hazitatumika tena, hivyo
wanalazimika kuzitupa, hiyo siyo kweli.
No comments:
Post a Comment