Familia ya NMB ikiwa ikiwa katika sherehe yao ya siku ya familia iliyofanyika kwenye ufukwe wa South Beach Hotel Kigamboni jana kama wabavyoonekana watoto wa Familia za wafanyakazi wa benki hiyo wakiogelea na kushiriki michezo mbalimbali iliyoandaliwa kwa ajili ya burudani ya siku hiyo
Watoto wa Wafanyakazi wa NMB kutoka Matawi mbalimbali jijini Dar Wakiwa katika michezo mbalimbali ndani ya hotel ya Southe Beach Kigamboni katika Siku ya familia ya NMB
Baadhi ya wafanyakazi wa NMB wakiwa na Familia zao katika siku ya familia ya NMB iliyofanyika jana katika Hotel ya South Beach Kigamboni
Muda muafaka wa Maakuli, Wafanyakazi na Familia zao wakiwa katika foleni ya Chakula wakati wa kusherehekea siku ya familia ya NMB iliyofanyika jana Kigamboni katika hotel ya South Beach
Kutoka Kushoto ni Dafrosa Mkami kutoka NMB Mwenge akifuatiwa na Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano Bw Iman Kajula, Mkuu wa Kitengo cha Benki Binafsi Bw Abdulmajid Nsekela na Mmiliki wa Lukaza Blog ambaye pia ni Mfanyakazi Wa NMB Songambele Bw Josephat Lukaza wakiwa katika Picha ya Pamoja katika Siku ya Familia ya NMB iliyofanyika Jana katika Hotel ya South Beach Kigamboni
Dafrosa Mkami (Wa Kwanza Kushoto) Kutoka NMB Mwenge akiwa katika picha ya Pamoja na rafiki zake katika siku ya familia ya NMB iliofanyika jana Katika hotel ya South Beach Kigamboni
Wadau wa NMB wakiwa katika Picha ya Pamoja wakati wa sherehe ya siku ya familia ya NMB
Muimbaji Mahiri kutoka SKYLIGHT BAND Aneth Kushaba aka AK 47 akiimba kwa hisia wakati alipokuwa akitoa burudani ndani ya siku ya familia ya NMB iliyofanyika jana Kigamboni
Anneth Kushaba aka AK 47 wa SKYLIGHT BAND na timu yake nzima ikitoa burudani ndani ya siku ya familia ya NMB iliyofanyika South Beach Kigamboni
Hapa ndipo bendi ya skylight ilipoweka makazi yake jana kabla ya kuanza kutoa burudani kwa familia ya NMB zilizofika katika siku ya familia ya NMB
Ngongoti naye hakuwa nyuma katika kuyarudi mangoma kutoka kwa bendi ya Skylight
Aneth Kushaba aka AK 47 akikata mauno haswa wakati bendi ya Skylight ilipokuwa ikitoa burudani kwa familia za NMB zilifika katika sherehe ya siku ya familia ya NMB iliyofanyika jana
Mary Lucas wa skylight bendi akicheza na shabiki wake ndani ya hotel ya south beach wakati wa siku ya familia ya NMB.
No comments:
Post a Comment