Saturday, December 22, 2012

MKUTANO WA CCM WAFANA MBEYA LICHA YA KUTAWALIWA NA USHABIKI WA KISIASA SUGU AWATULIZA WAFUASI WAKE WASILETE FUJO KWENYE MKUTANO HUO

=

Baadhi ya wananchi na wapenzi wa CCM Wilaya ya Mbeya Mjini wakiwa katika mkutao huo uliyofanika katika kiwanja cha kabwe mwanjelwa




Hapa Naibu Waziri wa Elimu Mhe.Mulugo akiongea na wananchi na wapenzi wa ccm huku akielezea sera za chama cha mapinduzi na mikakati yake

 M/Kiti wa CCM Mkoa wa Mbeya Mhe.Godfrey Zambi(mb),akiwasalimia na kuwahutubia wananchi na wanaCCM wa Mbeya Mjini hiyo jana

Viongozi mbalimbali wachama walikuwepo mkutanoni hapo
Vituko vimeanza hapa mkuu wa wilaya Mbeya Norman Sigalla akipokwea na wafuasi wa chadema upande wa pili wa barabara kuu iendayo tunduma
Mashabiki wa chadema wanamshangilia mkuu wa wilaya hiyo huku wakimfuta na kumwambia njoo huku tuna sera nzuri
Mkuu wa wilaya huyoo anatimkia kwenye mkutano wao wa ccm
Anavuka barabara kuelekea mkutanoni baada ya kuwaacha hoi washabiki wa chadema
Ngoma inogile sasa sugu anapita barabarani wafuasi wa chama cha chadema wanamzuia ashuke hapo kwenye mkutano wa ccm 
Kazi kweli kweli ushabiki wa kisiasa hapa barabara imefungwa kwa muda
Mashabiki wa chadema wazuia kabisa sugu asipite na ashuke eneo hilo
Hakika mweshimiwa mbunge wa mbeya mjni Joseph Mbilinyi ameshuka kwa hasira toka katika gari yake ili aongee na wafuasi wa chadema

Sugu akiwaambia wapenzi na mashabiki wa chaedema jamani naombeni sana waacheni wenzetu wa ccm wafanye mkutano wao kwa amani tusiwazuie tafadhalini sana hebu tuwe wastaarabu kwa hili huku akishangiliwa

Sasa naombeni njia nirudi zangu home kwani nimechoka nimetoka kikaoni wapendwa acheni fujo naombeni niachieni njia niende
Jamaa wamekubali wamemwachia njia
Sugu huyooo anaenda zake
Matukio yote haya yametokea jana katika kiwanja cha kabwe jijini Mbeya

Picha na Mbeya yetu

No comments:

Post a Comment