MABUSU NI SUMU KWA WATOTO WADOGO
Mabusu
kwa watoto ni hatari: Wataalam wa afya nchini wametahadharisha wazazi
kuwa macho na watu wanaobusu na kuwabeba watoto wao wachanga, wenye umri
chini ya miaka mitano, kwa kuwa wanachangia kwa sehemu kubwa
kuwaambukiza maradhi ikiwemo nimonia.
Watu wametahadharishwa kuwa ikiwa wanataka kuwabusu na kuwashika watoto, wahakikishe kuwa, mikono yao imesafishwa na uso pia kabla ya kuwashika watoto ili kuweza kupunguza idadi ya watoto 15000 wanaokufa kila mwaka kutokana na ugonjwa wa Nimonia.
Hayo yamesemwa na Ofisa Mfwatiliaji wa Magonjwa ya Watoto, yanayokingwa kwa chanjo kutoka Wizara ya Afya Dk, Daudi Manyanga alipotoa Somo kuhusu Nimonia wakati wa Semina iliyowausisha waandishi wa habari.
Habari via Habari leo
No comments:
Post a Comment