Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara akiongea
jambo na Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Maendeleo Vijana James
Kajugusi (aliyevaa suti ya blue) jana mara baada ya kumaliza
kuwatembelea vijana wajasiriamali wa soko kuu la jijini Mwanza ambao
walipata mkopo kutoka mfuko wa vijana kupitia Halmashauri ya jiji.
Waziri Dk. Mukangara aliwatembelea wajasiliamali hao ili kuona fedha
walizopata zimewasaidiaje kama kundi la vijana na kijana mmojammoja.
Mwenyekiti
wa SACCOS ya Wafanyabiashara Wadogowadogo Mkoa wa Mwanza (WADOKI)
Mussa Ally akimuonyesha Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Dk. Fenella Mukangara (kulia) mfano wa jengo wanalolitarajia kujenga
hivi karibuni kama kitega uchumi chao jana jijini Mwanza. SACCOS hiyo
ilipata mkopo kutoka mfuko wa vijana mwaka 2009 fedha ambazo
waliwakopesha vijana wanachama 12.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara
(katikati) akimsikiliza Jummanne Izengo (kulia) ambaye alimueleza jinsi
alivyonufaika na mkopo alioupata kutoka mfuko wa vijana ambao
umemuwezesha kununua mashine ya kusaga nafaka, kulia ni Mkurugenzi
Msaidizi kutoka Idara ya Vijana James Kajugusi . Waziri Dk. Mukangara
alimtembelea Izengo jana katika eneo lake la biashara lililopo Mwaloni
jijini Mwanza ili kuona fedha alizopata zimemsaidiaje kama kijana.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara
(kushoto) akiongea jambo na Songaleli Mzee (kulia) ambaye ni
mfanyabiashara wa soko kuu la jijini Mwanza aliyepata mkopo kutoka mfuko
wa vijana na kufanya biashara ya nafaka. Katikati ni Edward Kabululu
ambaye ni Mwenyekiti wa Mwanza SACCOS ambayo ni moja kati ya 14 za mkoa
wa Mwanza zilipata fedha za vijana mwaka 2009 na kumpatia mkopo Mzee.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara
(katikati) akiongea na wafanyakazi wa SACCOS ya Wafanyabiashara
Wadogowadogo Mkoa wa Mwanza (WADOKI) jana jijini Mwanza juu ya umuhimu
wa kuwahimiza wanachama wao hasa vijana kuitumia mikopo wanayoipata
katika shughuli za kilimo cha chakula, ufugaji wa samaki na uvuvi ili
kuisaidia nchi kuepukana na tatizo la njaa. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi
kutoka Idara ya Maendeleo ya Vijana James Kajugusi na kushoto ni
Mwenyekiti WADOKI SACCOS Mussa Ally.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kulia)
akimuangalia mteja akisukwa nywele katika Saluni ya Juvee Kanuzile
(hayupo pichani) ambaye alipata mkopo kutoka mfuko wa vijana kupitia
halmashauri ya jiji mwaka 2009 na kufanya biashara ya saluni. Waziri Dk.
Mukangara alitembelea saluni hiyo ili kuona fedha alizopata Kanuzile
zimemsaidiaje kama kijana.
Picha na Anna Nkinda – Maelezo
No comments:
Post a Comment