Mwanafunzi akiwa ameuchapa usingizi nusu saa tu baada ya mtihani kuanza. |
Wanafunzi hawa walianza kusinzia mmoja mmoja ilipogonga nusu saa tu baada ya muda wa kuanza mtihani ambao ulipangiwa saa mbili. Wanafunzi walionekana kuwa hoi huku wengi wakizikusanya karatasi zao za mitihani bila ya kuandika majibu ya maswali zaidi ya matatu.
wavuti.com inayo video inayoonesha wanafunzi karibu wote wakiwa wamesinzia, ila kwa sababu za kimaadili, video hiyo haitawekwa hapa ili kuwasitiri baadhi ya wanafunzi ambao sura zao zinaonekana dhahiri.
Ikiwa unataka maelezo ya ziada, tafadhali wasiliana na MohamediMtoi
Wanafunzi wote wakiwa wamelala darasani |