Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina
la TIENA MWAZEMBE mwenye umri wa miaka 28 mkazi wa kijiji Hangomba kata
ya Bara wilayani Mbozi mkoani Mbeya amenusurika kufa baada ya
kutumbukia chooni wakati akifanya mapenzi huku mumewe akiwa maututi
chumbani.
Habari za uhakika kutoka kijiji hapo zinadai kuwa
mwanamke huyo licha ya kuwa mke wa mtu alikuwa anafanya ngono chooni na
WASI MGALA wakati mumewe akiwa ndani anaumwa na kwamba alidumbukia choo
baada ya banzi alilokuwa amekanyaga kukatika wakati wanafanya tendo
hilo.
Mwanamke huyo alidumbikia kwenye choo chenye urefu wa
futi 17 na kwamba baada ya kudumbukia, mwanaume aliyekuwa naye chooni
wakifanya ngono alikimbia na kumwancha mwanamke huyo akipiga kelele za
kuomba msaada ndipo wananchi walifika na kufanikiwa kumtoa ndani ya
shimo na kukimbiza kwenye dula la madwa linalomilikiwa na muuguzi
LEONARD NZOWA ambaye alitoa huduma ya kwanza kabla ya kumfika katika
hospitali ya Mbozi Mission.
Hata hivyo mume wa mwanamke huyo
SAIKI GODFREY KAROTI amesema kitendo kilichofanywa na mkewe ni cha
uzalilishaji na si cha uungwana.
Habari via Bongo clan