Sisi wanafunzi wa kitanzania nchini Urusi, tunakosa huduma za msingi kama vile malazi , chakula na bima ya afya.
Serikali kupitia bodi ya mikopo ya elimu ya juu na Wizara ya Elimu
na mafunzo ya ufundi ,kwania njema iliamua kusomesha wanafunzi wa
kitanzania katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo Urusi.
Lakini kutokana na utendaji mbovu na ubinafsi wa baadhi ya watendaji wa
Bodi ya mikopo, kumekua na ucheleweshwaji wa ulipaji wa pesa za
kujikimu , malazi na bima ya afya kwa zaidi ya miezi mitatu sasa bila
sababu za msingi toka kuanza kwa mwaka wa masomo 2012/13.
Hali
hii imetupelekea wanafunzi kuanza kufukuzwa katika hosteli tunazoishi
pamoja na kutopatiwa huduma za afya pindi tunapo ugua. Ikumbukwe kuwa
katika nchi za ulaya huwezi pata matibabu kama huna bima ya afya.
Shukrani zetu za dhati ziende kwa Ubalozi wa Tanzania nchi Urusi kwa
kushirikiana bega kwa bega na Wanafunzi katika kutafuta ufumbuzi wa
tatizo hili linalotukabili katika kipindi hiki kigumu pamoja na majuku
mengi waliyonayo, pamoja na jitihada hizo mpaka sasa hakuna ufumbuzi
wowote uliopatikana.
Tunaandika waraka huu kwa huzuni na
masikitiko makubwa sana kwa sababu kutopatiwa mikopo mpaka sasa sio tu
kunafanya wanafunzi waishi maisha magumu na hatari, vilevile kunatia
aibu Taifa kwa kutolipa ada kwa wakati.
Tunaamini kabisa
Serikali kupitia bodi ya mikopo ,wizara ya elimu na mafunzo stadi na
ufundi na ubalozi wa Tanzania Nchini Urusi una nia njema kabisa
kusomesha vijana wake nje ya nchi, ispokua tu kuna baadhi ya watendaji
wa bodi ya mikopo wamekua wazembe na kutowajibika kwani wamekua wakitoa
majibu ya uongo na jeuri kwa uongozi wa wanafunzi na maafisa wa
ubalozi wa Tanzania nchini Urusi.
Ombi letu kwenu ni
kutufikishia ujumbe huu kwa wahusika na watendaji wa ngazi za juu za
bodi ili waweze kutusaidia sisi wanafunzi wa Urusi ambao tupo hatarini
huku ugenini.
Tunatumaini kutokana na Uzito wa tatizo letu
wahusika watalishughurikia na kulitatua tatizo hili kwa haraka zaidi na
kutupa ufafanuzi wa ucheleweshwaji wa mikopo ya wanafunzi kwa zaidi ya
miezi mitatu (3).
WANAFUNZI NCHINI URUSI.
No comments:
Post a Comment