Afisa uhusiano wa Tigo Marium Mlangwa akisema maneno ya
ufunguzi kabla ya Mkutano kuanza ambapo mkutano huo umefanyika leo katika
Hoteli ya JB jijini Dar es Salaam.
|
Kampuni ya Simu za Mkononi Tigo leo imezindua Promosheni itakayomuwezesha Mteja kununua simu Smartphone aina ya Ascend Y200 zenye ubora na kiwango cha hali ya juu na
kwa shilingi 175,000.
Meneja wa Internet Tigo akizungumza na waandishi wa habari leo
katika mkutano huo.
|
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam
leo Meneja wa Internet wa Tigo Bw, Titus
Kafuma amesema kuwa simu hizo zitakuwa zinapatikana katika maduka
yote ya Tigo nchini na kuongeza kuwa watakao nunua simu hizo watajipatia zawadi
mbali mbali ikiwemo kifurushi cha mwezi
mzima cha Smart Card, muda wa maongezi
wa shilingi 30,000 zitakazomuwezesha kupiga simu mtandao wowote nchini
na baadhi ya nchi nyingine za kimataifa.
Bw, Kafuma amesema kuwa katika kufanikisha swala hilo kampuni ya HUAWEI ambapo ndio waliotengeneza simu hizo.
Mkurugenzi Mtendaji
wa HUAWEI akizungumza katika mkutano huo.
|
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Bw Bruce Zhang amesema kuwa simu hizo ni nzuri na zina ubora
wa hali ya juu na kwamba zitamuwezesha mtumiaji kupata huduma zote za kisasa.