Serikali ya Malawi imesitisha
rasmi mswaada wa sheria ya kupinga mapenzi ya jinsia moja na polisi
wameagizwa kutowakamata watu wanaojihusisha na vitendo vya ushoga mpaka
uamuzi mwingine utakapotolewa.
Mapenzi ya jinsia moja kwenye
nchi ya Malawi yalipigwa marufuku na kutolewa kifungo cha miaka 14 jela
kwa wanaokamatwa kushiriki na siku kadhaa zilizopita baadhi ya viongozi
wa kimagharibi wametishia kusitisha kuzipa msaada nchi za Afrika ambazo
zinakataa kutambua haki za mashoga.
Mmoja wa viongozi wa kijamii
mwenye ushawishi mkubwa anaeitwa Kaomba, amiomba serikali kutoruhusu
bunge kubadili sheria zake kuhusu ushoga huku akisema ni kinyume na
maadili.
BBC Swahili wamesema mwandishi
wao ambae yuko Blantyre anasema kuwa kusitisha kwa muda sheria hiyo,
kutawaudhi sana watu wengi hasa viongozi wa kidini pamoja.
Kama unakumbuka… mwaka 2010
wanaume wawili walikamatwa na kushtakiwa kwa utovu wa nidhamu hadharani
baada ya kusema wataoana ambapo hiyo kesi ilikua kero kwa mataifa
yanayosupport hizo ndoa za jinsia moja na hata kusababisha baadhi yao
kusitisha msaada kwa Malawi, na ikawa pigo kubwa kwa nchi hiyo ambayo ni
moja ya nchi maskini zaidi duniani.
Rais wakati huo akiwa Bingu wa
Mutharika aliwasamehe wanaume hao kwa misingi ya kibininadamu ingawa
alisisitiza kuwa ni kinyume na maadili ,na hata tamaduni za kiafrika na
sheria za nchi.
Hata hivyo rais Joyce Banda
aliyemrithi Bingu amewaambia wabunge kwamba anataka kubatilisha sheria
hiyo na kuhalalisha mapenzi ya jinsia moja.