Mtu yeyote anayepata walu mlo mmoja kwa siku na kupitisha kati ya siku moja au tatu bila kupata choo, anatatizo la kukosa choo (Constipation), pia kupata choo kigumu na maumivu makali ama kufikia kutoa choo kama mbuzi wakati mwingine kikiwa na matone ya damu ni dalili za tatizo hili la kukosa choo.
"Tafiti zinaonesha kuwa mtu anaweza kupoteza maisha iwapo atakosa choo siku tano mpaka saba mfululizo"
Sababu za kukosa choo ziko nyingi ikiwa ni pamoja na:-
•Kukosa mlo kamili ama kula vyakula viingi vyenye kiwango kikubwa cha wanga na mafuta,
•Kula vyakula vilivyokobolewa na vilivyo changanywa na madawa ili visiharibike,
•mifumo hatarishi ya maisha (Dangeraous Lifestyles) kama vile matumizi ya pombe na sigara kwa wingi,
•Ukosefu wa kiwango cha kutosha cha mbogamboga na matunda katika milo yetu,
•Maji yasiyo salama,•Kuvuta hewa chafu,n.k
Hizi ni baadhi tu, na hadhari zake zaweza kuwa:-
•Chakula kutomeng'enywa vizuri (poor function of digestion system)
•Maumivi makali wakati wa kupata choo,
•Uchafu uliokaa muda mrefu kugeuka sumu,
•Bakteria wenye madhara kuzaliwa na kuathiri utumbo mpana na viungo vingine mwilini.
Hii yaweza sababisha magonjwa sugu kama: •Saratani ya utumbo mpana (Colon Cancer)
•Presha (Arteriosclerisis)
•Kuongezeka uzito (Obesity)
•Tumbo kujaa gesi
•Magonjwa ya Ini
•Figo kushindwa kufanya kazi vizuri,
•Magonjwa ya ngozi,
•Kukakamaa kwa mishipa ya damu,
•Kisukari,
•Magonjwa ya moyo n.k