Friday, November 16, 2012

MAONYESHO YA VIFAA VYA UJENZI MAARUFU KAMA TANZANIA BUILDING EXPO YAZINDULIWA RASMI JIJINI DAR ES SALAAM

Maonyesho ya  Vifaa vya Ujenzi  kwa mara ya kwanza yamezinduliwa leo jijini Dar es Salaam na Katibu mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bi, Joyce Mapunjo ambapo  yatakuwa ni maonyesho ya Siku tatu ambapo tamati yake itakuwa ni jumapili.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Bihashara Bi, Joyce Mapunjo akisoma hotuba yake wakati akizindua maonyesho hayo ambapo amewataka watanzania kununua vifaa vinavyozalishwa na viwanda vyetu vya hapa hapa nchini Tanzania.
Bi Mapunjo amevipongeza viwanda vya Tanzania na kusema kuwa sasa wanajivunia kwani kuna wingi wa Bidhaa zinazo zalishwa hapahapa Tanzania vinavyouzwa Nje ya Nchi.
Na amevitaja baadhi ya Vifaa hivyo kuwa  ni Nondo na Cement.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Bihashara Bi, Joyce Mapunjo akikagua baadhi ya Vifaa katika kampuni ya  Sitta Steel Rolling, LTD inayozalisha vifaa vya Maji.

Katibu mkuu akikagua moja ya Jenereta linalozalishwa katika kiwanda chaPhoenix hapo akiwa na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Bw, Oussama Fayad

No comments:

Post a Comment