Sunday, November 4, 2012

MALALAMIKO KWA CRDB NA M-PESA FEKI

Kero hii ameiwasilisha Lemburis Kivuyo kwenye kundi la WanaMabadiliko.
---

Kila nikiingiza pesa kwenye akaunti yangu saa nyingine huingizwa manually baada ya siku 5, nini maana ya huduma hii sasa. Na mara nyingine mpaka ufuatilie benki kwa miguu ndipo wakuingizie.  

Hivi hawa watu wanaziingiza hizi teknolojia bila kujiandaa au wanafanya makusudi ili watuibie 

Kesi moja ya tarehe 25 Oct 2012. Niliingiza kama Tsh 50,000 ambazo zilikuja ingizwa tarehe 30, Oct 2012  halafu nikaulizia salio hakuna, nikarudia kila baada ya kama dk 20 mara 7 hakunba, mara zote hizo nakatwa sh 10 kwa kila ulizo.  

Mimi kwa kweli nimeboreka na kuumizwa na jinsi mashirika haya yanavyotuchezea akili Watanzania. Mimi nilifurahia hii huduma kuondoa ukiritimba wa kwenye foleni ndefu na nyingine mpaka saa tatu ukiwa kwenye foleni ndipo upate huduma, sasa kwenye mitandao ndiyo siku tano na makato juu. Tunakwenda wapi?

Kwenye mwezi wa nane niliweka pesa kwa mtindo huohuo kama TZS. 200,000/= zikatolewa halafu baada ya kufuatilia sana zaidi ya wiki 2 zikarudishwa.

Nimeweka Shs 40,000 tangu jana usiku ambazo mpaka sasa hazikuwekwa kwenye akaunti yangu. Nikiwapigia kwa namba ya 0714197700 na 0755 197700 hazipatikani na mara chache zinapopatikana unaambiwa ziko busy.
 
Wadau jamani mnisaidieni hapo.

Hakuna mwanya wa kisheria wa kuwashitaki hawa wezi wa pesa zetu?

----
Lemburis Kivuyo
+255654650100/078 7665050/0755646470