Kwa upande wake mwanasheria wake ambaye alisema lengo la kukutana na waandishi wa habari ni kuweka ‘record’ sawa tofauti na watu walivyolisikia tuki hilo, alidai kuwa tarehe 20 mwezi uliopita Lord Eyez alipigwa simu na mtu ambaye walikuwa wamefahamiana kwa muda mfupi na kuamini kuwa alimtaka kwenda kuzungumza masuala ya kijamii.
Alipofika katika eneo hilo ambapo ametaja kuwa ni Kinondoni, Lord Eyez alikutana na kundi la watu ambapo wawili anawafamu lakini alidai hawezi kuwataja kwasababu za kisheria. Alisema baada ya muda mteja wake alivamiwa na watu kama 15 waliokuwa kwenye magari matatu ambao walisema wanamshuku kuiba vifaa vy gari na kumweka chini ya ulinzi kwa masaa yasiyopungua matatu huku wakimshinikiza akiri kuhusika na wizi wa vifaa hivyo.
Baada ya hapo ndipo alipopelekwa polisi. Mwanasheria huyo alidai kuwa Lord Eyez aliwekwa mahabusu kwa zaidi ya siku 10 kitu ambacho ni kinyume cha sheria kwa mtuhumiwa kukaa bila kupelekwa mahakamani.
Aliongeza kuwa si jambo jema kwa wananchi kuhitimisha kwa kudai kuwa tayari Lord Eyez ni mhalifu na amehusika kwenye tukio hilo kwakuwa bado mahakama haijaamua hivyo.
“Jamii itoe nafasi kwa mchakato huu wa kisheria uweze kutoa majibu, majibu hayo ndio watu wanaweza kuyafanyia kazi,” alisisitiza.
Amesema taarifa hizo zimemwathiri mteja wake hasa kwakuwa anategemea zaidi mapokeo chanya ya mashabiki wake ili kazi zake ziweze kufanikiwa hivyo ana haki ya kuendelea kuitwa mtuhumiwa tu wa jambo hilo.
Amesema yeye na mteja wake wanafikiria kuandaa mchakato wa kisheria ili kuwashughulikia wale waliohusika na kusambaza habari za kumchafua kimakusudi wakati ambapo vyombo vya sheria havijatoa uamuzi sahihi.
Kwa upande wake Lord Eyez amewataka mashabiki wake wake na subira wakati ambapo mahakama inaendelea na mchakato wa kutoa maamuzi yake.
Naye Nikki wa Pili alidai kuwa tukio hilo limewaweka Weusi katika wakati mgumu kwakuwa wamekuwa wakisumbuliwa na watu wengi kutaka walizungumzie suala hilo lakini wamekuwa kimya kwakuwa walitaka lizungumziwe kisheria zaidi.
No comments:
Post a Comment