Katibu mkuu ofisi ya waziri mkuu Bw, Peniel Lymo akizungumza
katika mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali wa kupambana na janga la ukimwi
ulioandaliwa na TACAIDS ambapo alisema kuwa
wananchi wanatakiwa kuzingatia ushauri na kuepukana na vishawishi vibaya
vinavyochocea maambukizi ya VVU.
Amesema kuwa vijana wanatakiwa wahakikishe kuwa janga hili
la ukimwi linaondoka kwani anauhakika kuwa vijana wanaweza kwakuwa wao ndio
kila kitu.
Bw, Lymo alisisitiza
Mashirika yanayojishughulisha na kupambana na Janga la UKIMWI kuhakikisha kuwa pesa zote zitakazotolewa kwa
mashirika mbalimbali kwa ajili ya kusaidia kupunguza janga hili la ukimwi
zitumike sawasawa kwa matumizi ya kuzuia UKIMWI na sio vinginevyo.
|
No comments:
Post a Comment