Thursday, October 4, 2012

WALIMU WAMUOMBA KIKWETE AINGILIE KATI MATATIZO YAO WAKATI WA MAADHIMISHO YA SIKU YA WALIMU DUNIANI INAYOFANYIKA KESHO ULIMWENGUNI KOTE

Raisi wa Chama cha walimu CWT akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari leo katika makao makuu ya Chama hicho jijini Dar es Salaam.
Katika  kuadhimisha siku ya Walimu Duniani  inayotarajiwa kufanyika Kesho October 5  mwaka huu ulimwenguni Chama cha walimu Tanzania kimumeumba Rais wa Tanzania Dr Jakaya Mrisho Kikwete kushughulikia Matatizo ya Walimu kama anavyo ahidi huwa katika hotuba zake kila anapo alikwa kuwa Mgeni Rasmi.
Rais wa Chama cha Walimu Tanzania Bw, Gratian Mukoba  amesema kuwa, ni ahadi nyingi sana ambazo Mh Rais amezitoa katika mwaka 2006 na 2010 lakini walimu mpaka leo hawajaona Dalili yoyote ya serikali kuzitekeleza licha ya kwamba miaka miwili imepita.
Amesema kuwa Hali ya Walimu wa Kitanzania  imedorora kwani Tanzania ndiyo nchi pekee inayowalipa walimu mishahara Duni ukilinganisha na Kenya, Uganda na Rwanda.
Kauli Mbiu ya siku ya walimu Duniani ni ‘’Stand for Teachers’’ inayotafsiriwa kwa Kiswahili kuwa ni ‘’Kuwatetea walimu’’.