Saturday, October 6, 2012

WAKATI WENGINE WAKILIA NA UGUMBA,WENGINE WAMEKUWA WAKIJIFUNGUA NA KUWATUPA WATOTO WAO

Mtoto aliyeokotwa

Binti  aliyefahamika kwa jina la lina akiwa amembeba kichanga huyo


MTOTO mchanga anayekadiriwa kuwa na umri wa mwezi mmoja amekutwa ametupwa kwenye boma la nyumba moja iliyopo katika kata ya Ibisabageni wilayani Sengerema mkoani Mwanza.

Tukio la kuokotwa kwa mtoto huyo limetokea siku ya Jumatatu muda wa asubuhi ambapo mtoto huyo alikutwa ametelekezwa na ndipo msamara mwema aliaamua kutoa taarifa kwa ndugu jamaa ambao waliofika eneo la tukio.

Akielezea kuhusu tukio hilo amesema kuwa wakati anapita eneo hilo alisikia sauti ya mtoto ikilia  na ndipo aliposogea karibu na kukuta mtoto huyo mchanga akiwa amelazwa chini.

Naye Afisa Mtendaji wa kata hiyo Bw. JAPHET MASHALA  ambaye alikuwepo eneo la tukio amelaani kitendo hicho na kusema ni cha kinyama na kuwaomba wananchi kuwa na moyo wa ubinadamu wa kuthamini maisha ya wengine kwani mtoto huyo hana hatia yoyote.

Jhudi za kumtafuta aliyemtelekeza mtoto huyo zilikuwa zinaendelea.


Taarifa ya PAULINA E. MPIWA wa SENGEREMA via FPluss