MWANAFUNZI aliyemaliza kidato cha sita katika shule ya sekondari
Saronge, iliyoko mkoani Kigoma na kuchaguliwa kwenda chuo kikuu cha UDSM kwa
ajili ya kuanza masomo ya mwaka wa kwanza katika kipindi cha mwaka
2012/2013, amekufa akidaiwa kujinyonga wilayani Bunda mkoani Mara.
Tukio
hilo lilitokea juzi katika kitongoji cha Kimanitwentemi, kilichoko
katika kijiji cha Kabasa wilayani hapa na Mwenyekiti wa kitongoji hicho
Donard Kalemela, alisema mwanafunzi huyo anatambuliwa kwa jina la
Majinge Mafuru, mkazi wa kijiji hicho.
Baba
wa mwanafunzi huyo, Samson Musimu, alisema mwili wa mwanafunzi huyo
uligunduliwa na mdogo wake baada ya kutoka shuleni na kuingia ndani ya
nyumba hiyo.
Alisema mfukoni mwake
walikuta ujumbe wa maandishi ukisomeka, “Naomba mniandalie mahali pa
kulala, nimeamua mwenyewe, baada ya kuwa nimeghafirika, msimshuku mtu
yeyote, ni maamuzi yangu mwenyewe, ahsante.”