Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imeishauri Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar kuwatafuta, kuwakamata wale wote walioshirikia katika
vitendo vya vurugu iliyotokea wiki iliyopita; Na, kuvunja vikundi vyote
vya kihalifu vilivyoanza kushamiri Zanzibar.
Aisha, Tume imeitaka Serikali kujipanga kikamilifu na kuhakikisha kutokurudiwa tena kwa viteondo kama hivyo nchini.
Taarifa
iliyotolewa na Tume hiyo na kutiwa saini na Kahimshina wake, Zahor J.
Khamis, imeeleza kwamba vitendo hivyo ni uvunjaji wa haki za binadamu na
vinapingana na sheria za nchi na ni kinyume na masharti ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT).
Hivyo, Tume
inalaani kitendo cha kuuawa kwa askari Said Abrahmani, kwani kitendo
hicho ni uvunjaji wa haki za binadamu na kinapingana na sheria za nchi
na ni kinyume cha katiba ya JMT Ibara ya 14, inayozungumzia ‘Haki ya
Kuishi’ na Katiba ya Zanzibar, Ibara ya 13 inayozungumzia ‘Haki ya Kuwa
Hai’.
Kitendo hicho pia kinapingana na Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Binadamu namba 3 na ule wa Afrika, Ibra ya 4.
Hivyo,
imeendelea kushauri Serikali pamoja na Vyombo vya Ulinzi na Usalama,
kufanya uchunguzi wa kina kuwatamhua na kuwakamata wahusika wote wa
mauaji hayo na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
Aidha,
Tume hiyo imelaani kitendo alichofanyiwa Diwani wa CCM wadi ya Chumbuni
kwa kushambuliwa na kujeruhiwa, kitendo ambacho kinakwenda kinyme na
haki za hinadamu na Katiba ya Tanzania, Ibara ya 12(6) (C) na Katiba ya
Zanzibar, Ibara ya 13(3) inayopiga marufuku mtu kuteswa, kuadhibiwa
kinyama au kupewa adhabu za kumdhalilisha.
Pia, kupora mali mtu ni kinyumea cha sheria chini ya Ibara ya 17, ya JMT na Ibra ya 16 inayozungumzia haki ya umiliki.
Tume
imeendelea kuwaleza kuaw matukio yote hayo ni mwendelezo wa matukio
kadhaa yaliyotokea hapo awali na ambapo yalitamkwa hadharani tena bila
kificho, matokeo yake ndiyo yaliyotufikisha leo hapa tulipo. Hayo ni mapungufu ya uzingatiaji wa Misingi ya Utawala Bora ikiwemo Uwajibikaji na Utawala wa Sheria.
Ikielezea
utata uliojitokeza katika kadhia ya kutoweka kwa Sheikh Farid, tume
hiyo imeeleza kwamba kumejitokeza kwamba Jumuiya ya Uamsho ni ya kidini
(Kiislam) na imekuwa ikitumiwa na makundi ya wahuni ambayo
yamejipachika majina kama mbwamwitu, simba mkali, ubaya ubaya na toto
tundu ili kufanikisha azma yao.
Dai la kutekwa kwa
Sheikh Farid lina utata mkubwa ambao unahitaji uchunguzi na ufafanuzi
kama vile huko alikotekwa vipi aliweza kufika msalani (chooni) ambako
alikuwa akinywa maji wakati akiwa amefungwa kitambaa usoni na mikononi
akiwa na pingu na katika nyumba ambayo haijui imekaaje na kushindwa
kuitambua muda wote.
Kunauhusiano gani wa kutekwa
kwa kiongozi wa Uamsho na hujuma za mali za watu na CCM na lile dai la
kunyimwa kula kwa siku tatu bila kuathirika kiafya.
Hivyo
taarifa hiyo ilimtaka Sheikh Farid kutoa maelezo yanayothibitisha
pasipo na mashaka ili kuwathibitishia wazanzibari, watanzania na
ulimwengu kwa jumla juu ya kutoweka kwake.
Sheikh
Farid anadai alitekwa na watu wasiojulikana tarehe 16 mwezi huu na
kuonekana siku tatu baadae akiwa katika hali ya uzima na salama jambo
ambalo lilisababisha vurugu kubwa hapa Zanzibar na kusita kwa shughuli
zote za kiuchumi na kijamii kutokana na fujo hizo zilizotokea ambapo
hadi sasa haijajulikana thamani au hasara iliopatikana kutokana na
machafuko hayo ambapo askari mmoja wa kikosi cha FFU kwa jina la Said
Abdulrahman kuuwawa.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELAZO ZANZIBAR