Na Veronica Kazimoto – MAELEZO
Dar es Salaam
18.10.2012.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Jakaya Kikwete amemteua
Prof. Mwajabu Possi kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam kuwa Mwenyekiti wa
bodi ya wakurugenzi ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kwa kipindi cha
miaka mitatu kuanzia tarehe 8 Octoba, 2012.
Kufuatia uteuzi huo, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt.
Fenella Mukangara amewateua wajumbe mbalimbali wa bodi hiyo ambao ni Dkt
Mariam Nchimbi, Gideoni Mbalase, Prof. Elizabeth Kiondo na Balozi Kassim
Mwawando.
Wajumbe wengine ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari -MAELEZO Assah
Mwambene, Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Salva Rweyemamu, Mkurugenzi
wa Idara ya Habari -MAELEZO Zanzibar Omary Chunda pamoja na Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania Clement Mshana.
Wakati huo huo Waziri Mkangara amemteua Christopher Gachuma kuwa
Mwenyekiti wa bodi ya Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya.
Aidha amewateua Pendo Malebeja, William Erio, Richard Ndassa, Lina Kessi,
Leornard Thadeo na Allen Alex kuwa wajumbe wa bodi hiyo.