Taasisi ya vyombo vya habari kusini Mwa Afrika Tawi la Tanzania(MISA
TANZANIA) umeendelea kuonyesha masikitiko yake kwa Serikali ya Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa kushindwa
kulifungulia gazeti la Mwanahalisi mpaka sasa pamoja na kuwa Ukweli
umegundulika kuwa yaliyosemwa na Mwana Halisi ni ya kweli kabisa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya uhuru wa
habari ya kutetea Gazeti la Mwanahalisi Bw, Marccosy Albanie, amesema kuwa,
Sababu walizotumia Viongozi wa Wizara ya Habari Kulifungia Gazeti la
Mwanahalisi sio za kweli kwani kilichoandikwa na Mwanahalisi ni ukweli mtupu ambao hivi karibuni
Umethibitishwa na Dk Steven Ulimboka.
Hivi Karibuni Dk Ulimboka kupitia kwa wakili wake Mheshimiwa
Nyororo Kicheere aliweka wazi kwamba
afisa wa Usalama wa Taifa Bw, Ramadhani Ighondu alihusika katika kutekwa
kwake kwakuwa mazingira yote kabla na
baada ya tukio hilo yanaonyesha kwamba Ramadhani Ighondu ni Mdau katika tukio
hilo.
Taarifa hiyo imesema kuwa inashangazwa sana na Serikali kwani badala ya kutoa tamko kwamba
imepata uhakika kuhusiana na aliyemteka na kumtesa Dk
Ulimbokana baadaye kumtupa katika Msitu wa Pande jambo ambalo Gazeti la
mwanahalisi lilisaidia kutoa ushahidi wa tukio hilo lakini bado serikali imekaa
kimya na Gazeti hilo bado limefungiwa.
MISA TANZANIA imeisisitizia Serikali kulifungulia Gazeti la
Mwanahalisi kwani tayari Dk Stephen
Ulimboka ameshaweka wazi kuwa
kilichoandikwa na Mwanahalisi ni cha Kweli kabisa na pia wameikumbusha serikali
kuwa swala hilo sio dogo katika anga za Kidemocrasia na haki za Binadamu.
Ameongeza kuwa kutolifungulia Gazeti la Mwanahalisi ni
kuwanyima wasomaji wa gazeti hilo kile wanachstahili kukisoma kwani Gazeti hilo
lilikuwa na wadau wake ambao walikuwa wanahabarika kupitia gazeti hilo.