Mbunge wa Iringa Mjini na Waziri kivuli wa Maliasili na
Utalii akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) leo jijini Dar es
Salaam ambapo amemtaka Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
jakaya Mrisho kikwete kumuwajibisha Waziri wa maliasili na Utalii Mhe,
Kagasheki kwa kuwa anaficha Majangili na pia anashindwa kusimamia na kulinda
wanyama wa Tanzania.
Msigwa amesema kuwa
Waziri Kagasheki ameonyesha Udhaifu mkubwa sana ndani ya Muda Mfupi Tangu akabidhiwe wizara
hiyo na Mhe, Rais na kuongeza kuwa
Waziri huyo anafanyakazi kazi ya kuhujumu nchi kwa kuwalinda wahalifu.
“Kagasheki kwa asilimia zote anaonyesha udhaifu wake kwa
kuwakumbatia Majangili wanao winda na kuuwa wanayama wa Tanzania, hivyo
Namuomba Rais, aingilie kati na kuchukua hatua ambazo waziri wake ameshindwa
kuzichukua”,amesema Msigwa.
Amesema kuwa jambo
linalompelekea aseme kuwa Kagasheke anawalinda Majangili ni kuwa Musigwa mwenyewe alitoa taarifa juu ya
udhaifu wa Waziri huyo kwa kushindwa kuwachukulia hatua Majangili pamoja na
kwamba Musigwa aliwataja baadhi ya wahalifu kwa majina lakini Waziri husika
amekaa kimya kana kwamba hilo ni jambo la Kawaida.
Amezungumzia pia juu
ya pembe za Ndovu zenye uzito wa tani 4 kutoka Tanzania na Kenya zilizoripotiwa kukamatwa Nchini Hong Kong hivi
karibuni huku zile zilizoibiwa kutoka
Tanzania zikiwa na thamani ya zaidi ya Sh, bilioni 2.5 na kusema kuwa hayo ni
matokeo ya Waziri dhaifu aliyopo katika Wizara hiyo.
“Waziri Kagasheki asipofanya kazi sawasawa nitahakikisha kuwa yanamkuta yaliyomkuta
Maige,” amesema Mch, Msigwa.
|