Meya wa Manispaa ya Ilala Bw, Jerry Slaa akizungumza na
wadau mbalimbali pamoja na walipa Kodi katika kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake
jijini Dar es Salaam, Katika kikao hicho meya
aliufahamishaUmma kuwa Manispaa yake imefanikiwa kukusanya kiasi cha 99%
cha mapato yake.
Meya amesema kuwa kwa ujumla ukusanyaji wa mapato katika
mwaka huu imepanda kutoka 88% kwa mwaka 2010/2011 mpaka shilingi 17.1
bilioni zilizokusanywa kwa mwaka huu
kiasi ambacho ni sawa ya 99% ya mafanikio ya Malengo.
“Ongezeko hili limetokana na vyanzo vingi vya mapato kwa
102% ambayo ni shilingi 2.25 bilioni kutoka katika mabango ya Matangazo
yaliyopo Barabarani” amesema.
Ametaja Kitengo kingine kilichochangia kuongeza mapato kuwa
ni Utoaji wa Leseni za Ujenzi kilichochangia Milioni 307 pamoja na Makusanyo ya Mapato kutoka kwenye kodi
yaliyochangia shilingi 2.14 bilioni .
|