Saturday, September 29, 2012

MFUASI WA CHADEMA ANUSURIKA NA KICHAPO BAADA YA KUTUMIA KITAMBULISHO CHA USALAMA WA TAIFA KUINGIA KATIKA MKUTANO WA CCM


Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Swila William akiokolewa na Askari katikati ya kundi la wana CCM baada ya kunusurika kupata kichapo na wanaccm kwa kosa la kuingia katika mkutano wa CCM kisirisiri wakati yeye ni Mtu wa CHADEMA.
Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa mwanachama wa CHADEMA ameijikuta katika wakati mgumu baada ya kuambulia kichapo kutoka kwa wanachama wa CCM baada ya kujipenyeza katika mkutano wao wa uchaguzi wa viongozi wa ngazi ya Wilaya.

Mtu huyo alijefahamika kwa jina la Swila William, mkazi wa Kalobe (50), na ambaye ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mshewe, amekubwa na masaibu hayo baada ya kuingia katika mkutano kwa kitambulisho cha ‘Usalama wa Taifa’ bila kujua kuwa anatambulika na baadhi ya WanaCCM.

Bwana William baada ya kuokolewa na askari wa kikosi cha jeshi la Polisi anashikiliwa kwa maelezo zaidi.

---
Habari na picha via blogu ya MalafyaleLeo
Bwana William katikati akitolewa nje na askari polisi