Kamati ya Olympiki Tanzania inatarajia kuwa na Uchaguzi Mkuu wa Viongozi wake wa Ngazi za
juu na chini kuanzia Tarehe 8/12/2012 mkoani Dodoma.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dae es Salaam
katika Ofisi za Kamati hiyo, Rais wa TOC Bw, Rashid Gulam amesema kuwa Uchaguzi huu unaofanyika kwa kipindi hiki ni
Muendelezo wa Uchaguzi kwani Uchaguzi
mkuu hufanyika kila Baada ya Olympiki
inapomalizika ina maana kubwa kuwa viongozi wapya watakaochaguliwa wawe na muda
muhafaka wa (miaka 4 ) katika maandalizi na timu zetu kwa ushirikiano na
Serikali.
Amesema kuwa Mgombea atakayegombea nafasi yoyote anatakiwa
awe na sifa zilizopo katika katiba ya TOC ikiwemo Awe mtanzania halisi na
anaweza kuongea Kingereza na Kiswahili sawa sawa.
Amewataka wagombea wenye sifa kwenda kuchukua Fomu katika Ofisi
za TOC Tanzania Bara na Zanzibar tarehe 25/10 na kurejeshwa tarehe 15/11 mwaka
2012.
Ameongeza kuwa Fomu zitauzwa
kwa shilingi 200,000(Rais, Makamu wa Rais, Katibu Mkuu na Naibu Katibu
Mkuu, Mhazini pamoja na Mhazini Mkuu msaidizi) na shilingi 150,000 kwa wale
watakaogombea nafasi za Wajumbe ambapo Fomu zote zitauzwa katika Ofisi za TOC.