Wednesday, October 17, 2012

DK ULIMBOKA AFUNGUKA:ASEMA ALIYEMPIGIA SIMU MPAKA AKATEKWE NI RAMADHANI IGHONDU AMBAYE NI AFISA WA USALAMA WA TAIFA

Baada ya kimya kirefu leo Leo Yule Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Dk Steven Ulimboka ametoa taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyosainiwa na wanasheria wake Shayo pamoja na Nyaroro Kicheere.

Taarifa yake imesema kuwa ameshangazwa na serikali kutomkamata mtu huyo ambaye ndiye aliyempigia simu na akamtaka wakutane naye  akatekwa na  amemtaja kwa jina la Ramadhani Ighondu afisa wa Usalama wa Taifa.

Amesema wakati anatekwa Dk alikuwa anatumia namba ya simu hii hapa 0713731690

Ulimboka amesema kuwa yupo tayari kutoa Ushirikiano endapo tume ya Kufanya uchunguzi itaundwa.