Na Queen Lema, ARUSHA -- Wanawake wa eneo la
Kisambare, Usariver, wilyani Meru mkoani Arusha wamesema kuwa kamwe
hawatavumilia kauli za mbunge wa jimbo hilo, Joshua Nasari badala yake
watalazimika kuingia barabarani kumpinga hadharani Mbunge huyo kwani
kauli zake hazijengi hoja za kutetea shida za wananchi na badala yake
zinachochea malumbano pamoja na migogoro huku wanawake wa Vijijini
wakiwa wanakabiliwa na shida mbalimbali
Wanawake hao waliyasema
hayo jana Wilyani humo wakati wakizungumza na Viongozi mbalimbali ambao
waliwatembelea Kijijini humo sanjari na kuongea na wanachama wa Chama
Cha Mapinduzi.
Walisema kauli za Mbunge wao siyo za kujenga bali
ni kubomoa na kuchochea malumbano makubwa ambapo kwa sasa alipaswa kuwa
anaongelea jinsi ya kutatua changamoto mbalimbali zilizomo kwenye jamii.
Wakasema
Mbunge huyo anapaswa kujua na kutambua kuwa alipewa jimbo hilo kwa
hasira kutokana na kukithiri kwa changamoto lukuki ambazo zimo kwenye
jamii hasa za Wameru na kwa hali hiyo huu ndio muda muafaka wa Mbunge
huyo kuhakikisha kuwa anatatua kero na wala sio kutoa matammko ambayo
hayana tija na jamii.
Waliongeza kuwa kauli hizo zimekuwa na
madhara makubwa sana hasa kwa vijana kwa kuwa mpaka sasa wapo baadhi yao
wanaofanya makosa na kuvuruga amani, kwa visingizo vya Mbunge huyo,
“tunachotaka kujua ni kuwa tunatatuliwa kero zetu lakini badala mbunge
afikirie suala zima la maendeleo yeye anafikiria kuzima mwenge wakati
sisi hatuna shida na mwenge na mwenge unapita lakini shida zetu hasa
sisi wakina mama wa Nkoakirika hatujui hata majira ya saa sasa tueleweje
kwani tukimbia CCM kutokan a na changamoto lakini hii ya sasa ni kali
na kama huyu mbunge ataendelea hivi basi ipo siku matatizo makubwa sana
yatatokea” waliongea akina mama hao huku wakilia.
Mbali na hayo,
waliongeza kuwa nao viongozi wa siasa watakiwa kukumbuka ahadi
mbalimbali ambazo wamezitoa kwa jamii hasa nyakati za kampeni kwani
baadhi ya viongozi, hasa wa Mkoa wa Arusha wakishapata nafasi ya
kuongoza basi wanakuwa na matamko ambayo hayana tija na badala yake
yanasabahbisha baadhi ya vijana kukamatwa ovyo na Polisi.
Awali
Katibu wa CCM Wilaya ya Meru, Langaeli Akyoo alikiri kuwa CCM ilikuwa na
kasoro hali ambayo iliwafanya wananchama wake kukopesha jimbo la
Arumeru Mashariki lakini kwa sasa chama hicho kimejipanga hata kwa
Watendaji wa huduma zote za kijamii kuhakikisha kuwa wanatekeleza sera
za wananchi.
Bw. Akyoo alisema, hasira ambazo ndio chanzo pekee
cha wananchi kutoa kura kwa upinzani kwa sasa zitapunguzwa kwa kiwango
cha juu huku jamii hasa za vijijini zenye mahitaji maalumu nazo
zikiweza kupatiwa ufumbuzi wa matatizo yao kwani uwezekano wa
kuwasaidia bado ni mkubwa sana.