Dk Ndugulile akifunua kitambaa kuashiria kutumika rasmi kwa
kisima cha maji katika shule hiyo baada
ya kuchangia kisai cha shilingi 2500,000/=zilizowezesha kuweka umeme jua katika shule ya sekondari
Charambe na kurahisisha huduma ya maji kupatikana.
Kufuatia huduma hiyo walimu na wanafunzi wa shule ya
sekondari Charambe waliahidi kuongeza juhudi katika kufundisha na kusoma kwa
kuwa hawatakuwa na hofu ya kukosa huduma ya umeme na maji ambayo awalli
walieleza kuwa ni kikwazo kwao katika kupata elimu bora pamoja na kuwa hatarini
kwa ajili ya magonjwa ya milipuko.
Pia Dk Ndugulile
aliyekuwa mgeni rasmi katika mahafali ya tatu ya shule hiyo alitembelea miradi
mbali mbali na kuwatunuku vyeti jumla ya wanafunzi 334 wa kidato cha nne.
|