Timu ya Vijana ya Simba ndiyo itakayoshiriki katika michuano
maalum ya Banc ABC Super 8 inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 4 hadi 18
kwa kushirikisha timu nane kutoka Tanzania bara na Visiwani.
Simba
imaemua kuipeleka timu ya vija na kutokana na timu ya wakubwa kuwa katika
programu nyingine kwa kipindi hicho.
Hata
hivyo taarifa hizo ni taarifa za wali lakini huernda mambo yakabadilika baada
ya viongozi wa Simba kukutana na TFF pamoja na waandaaji wa michuanio hiyo
kuzungumzia mustakabali mzima wa michuano hiyo yenye lengo la kuzinoa timu hizo
kabla ya kuyshiriki katika ligi kuu bara.
Banc
ABC imeingia mkataba wa miaka mitatu kwa ajili ya kudhamini michuano hiyo
itakayiokuwa ikipigwa katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid-Arusha, CCM
Kirumba-Mwanza, Taifa-Dar es Salaam na Amaan -Zanzibar.
|