Naibu
waziri wa Maliasili na Utalii Mh.Lazaro Nyalandu akisalimiana na viongozi wa
wilaya ya Meatu alipotembelea pori la akiba la Maswa.Nyuma yake ni mbunge wa
jimbo la Kisesa mkoa wa Simiyu.
|
Nyalandu akiongea na wananchi wa Maswa |
Naibu
waziri wa Maliasili na Utalii Mh.Lazaro Nyalandu (kulia) akiwa kwenye boti
akielekea kukagua hifadhi ya kisiwa cha Saanane jijini Mwanza. (Picha zote na Nathaniel Limu).
|
Serikali
imeahidi kutoa kiasi cha 6M/- kulipa fidia ya ng’ombe 22 wanaodaiwa kuuawa kwa
kupigwa risasi na askari wa wanyamapori wa pori la akiba Maswa wilayani Meatu,
mkoani Simiyu. Inadaiwa ng,ombe
hao walipigwa risasi na kuuawa Desemba 2009 baada ya kuingizwa kuchungia ndani
ya hifadhi hiyo, kitendo ambacho ni kinyume na sheria zinazolinda hifadhi za
wanyama pori . Ahadi hiyo
imetolewa juzi na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, wakati
akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na wakazi wa kata ya
Sakasaka jimbo la Kisesa. Alisema
lengo la uamuzi huo ni kuimarisha mahusiano mazuri kati ya askari wa
wanayamapori na wakazi wa vijiji vinavyozunguka akiba ya pori hilo. “Pia ni sehemu ya mikakati
inayochukuliwa na serikali ya kuhakikisha mgogoro wa muda mrefu kati ya uongozi
wa pori la akiba Maswa na wananchi wakazi wa vijiji vinavyozunguka pori
hilo,unamalizika na kurejesha amani na utulivu katika eneo hilo,” alisema
Nyalandu. Katika hatua nyingine,
Nyalandu ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Singida kaskazini, alisema kuwa
serikali inatarajia kuunda kamati huru ambayo itashughulikia kutafuta ufumbuzi
wa mgogoro uliopo kwa muda mrefu katika akiba ya pori la Maswa. “Katika kamati hii,kutakuwepo na
mwakilishi mmoja kutoka wizara ya mali asili na utalii na wajumbe watakaobaki
watakuwa ni watu huru ambao watazitendea haki pande zote mbili. Ni matarajio
yetu kwamba taarifa itakayotolewa na kamati hiyo haitaionea au kupendelea
upande wo wote, itakuwa timilifu,” alifafanua naibu waziri huyo. Nyalandu alisema kamati hiyo itatoa
taarifa yake wizarani mapema kabla bunge la sasa kuhairishwa. Katika hatua nyingine, alitumia fursa
hiyo kuagiza wananchi waendelee kuelimishwa vya kutosha juu ya sheria zote za
hifadhi za wanyama pori ili waweze kuzitii bila ya kushurutishwa. “Napenda kukumbusha kuwa marufuku
kuchungia,kulima,kuingiza au kufanya shughuli zo zote za kijamii ndani ya
hifadhi la wanyama pori. Mfugaji au mtu yeyote atakayevunja sheria halali
ailizowekwa atachukuliwa hatua kali za kisheria,” alisema Nyalandu. Awali Mkuu wa Wilaya ya Meatu,
Rosemary Kirigini, alisema hifadhi ya pori la akiba Maswa ipo kwa mujibu wa
sheria. “Kwa hiyo, wananchi
kuigiza mifugo yao ndani ya hifadhi hiyo kwa madai ya kutokuwa na maeneo ya
malisho ni kuvunja sheria. Tunashauri wananchi wenye mifugo wanaopakana na pori
la akiba la Maswa watafute maeneo mengine ya kupeleka makundi yao ya mifugo, au
washauriwe kupunguza mifugo yao kwa kuanzisha ufugaji wa kisasa,” alisema DC
Kirigini. Aidha, alisema kuwa
wataendelea kutoa elimu ya uhifadhi kwa madai kwamba hifadhi zilizopo, ni
hazina kwa vizazi vilivyopo sasa na vya baadaye kwa nchi ya Tanzania na dunia
kwa ujumla. Wakati huo huo, DC
Kirigini ameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kubadilisha jina la akiba la
pori la Maswa na kulipa jina la akiba ya pori la Meatu. Alisema kuwa kwa vile sasa wilaya ya
Maswa imegawanywa na kuwa na wilaya wilaya tatu baada ya kuanzishwa kwa wilaya
ya Bariadi na Meatu,akiba ya pori hilo ambalo sehemu kubwa ipo wilaya mpya ya
Meatu,hivyo kuna ulazima wa kuitwa pori la akiba la Meatu. Kwa upande wake Nyalandu alisema ombi
hilo la kubadilisha jina la pori hilo linazungumzika.Picha na story kwa msaada wa www.fullshangwe.blogspot.com