Thursday, August 2, 2012

MWAKEMBE;; NI MARUFUKU KUCHIMBA DAWA UKIWA SAFARINI

WAZIRI wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe amepiga marufuku tabia ya madereva wa mabasi ya kwenda mikoani kusimamisha magari porini kwa ajili ya abiria kujisadia (kuchimba dawa.) Akizungumza bungune wakati wa hotuba ya bajeti ya wizara yake Dk Mwakyembe amesema kwamba kitendo cha abiria kwenda kujisaidia porini ni kinyume na maadili ya watanzania na kinyume na haki za binadamu na kwamba ni hatari hata kwa afya za abiria wenywe.
“Hili suala mimi silikubali hata kidogo kwa sababu inashusha hesma, maadili ya watanzania, unakuta mzee wa miaka 50 na kuendelea anapeana mgongo na binti mwenye umri chini ya miaka 18,20 wakati wa kuchimba dawa”amesema Dk Mwakyembe na kuongeza:
“Ama mama mtumzima anapeana mgongo na kijana mwenye umri sawa na mtoto wake wakati huo wa kuchimba dawa kwakweli suala hili si halali hata kidogo na mimi siliafiki hata kigodo, naniseme kwamba kuanzia Desemba mosi mwaka huu basi itakayokamatwa imesimama kwa ajili ya abiria kuchimba dawa itapewa onyo kali kwa mara ya kwanza na mara ya pili itashitakiwa mahakamani”.

Katika hatu nyingine Waziri Mwakyembe alihitimisha hotuba yake kwa kuomba wabunge wapitishe bajeti hiyoo kwa kuwa ndiyo jibu la wizira hiyo.
"Waheshimiwa wabunge mwisho naomba muipitishe hii bajeti ndogo ili matatizo ya uchukuzi yapate ufumbuzi kwakuwa wizara hiii ilikuwa ICU"anasema Dk Mwakyembe.