Thursday, August 30, 2012
MSAFARA WA SAMUEL SITTA WAPATA AJALI
JANA tarehe 29/08/2012 Katika ziara Mheshimiwa Samwel Sitta Wazira wa
Jumuiya ya Afrika Mashari Kutoka Wilaya ya Karagwe kuelekea Wilaya ya
Kyerwa kulitokea ajali ya gari la Ofisa wa Ubalozi wa Tanzania Nchini
Uganda aliyekuja kuungana na Mhe. Sitta katika ukaguzi wa Miradi
mbalimbali inayotekelezwa chini ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Ajali
hiyo ilitokea muda wa saa 5:15 asubuhi katika eneo la Lukole katika Kata
ya Ihanda baada ya kuyumba na kuacha njia na kuangukia upande mmoja.
Katika ajali hiyo hakuna mtu yeyote aliyeumia wote Ofisa wa Ubalozi na
Dereva wake walitoka salama jambo ambalo halikuidhuru ziara ya Mhe.
Sitta na kuendelea mpaka Wilayani Kyerwa Murongo
