Monday, June 22, 2015

HII NDIYO KAULI YA WASIRA AMBAYE ANATARAJIA KUGOMBEA URAIS KATIKA MAJIBU YAKE KUHUSI WINGI WA WAGOMBEA URAIS KUTOKA CCM

36593
Watu ambao tayari wamejitokeza kutangaza kwamba Wanagombea nafasi ya kuwa wawakilishi wa CCM kwenye nafasi ya Urais idadi yao ni zaidi ya 35 mpaka sasa hivi... Waziri Steven Wasira amewasha kipaza sauti ndani ya Kikao cha Bunge Dodoma na kuongea hizi sentensi zake chache tu kwa wanaokosoa idadi hiyo ya Wagombea.
“Chama cha Mapinduzi ni Chama kikubwa wengine wako huko wananung’unika ooh kina Wagombea wengi mlitaka wawe wachache ili wawe wangapi? Ni wengi kwa sababu Chama chenyewe ni kikubwa, sio Chama kidogo ambacho Viongozi wake wakiingia kwenye Helicopter chini kunabaki hakuna Kiongozi” Steven Wasira.
“Tunapashapasha moto alafu mwisho wa yote tunapata Mgombea mmoja na tutasonga mbele, mwendelee kujiandaa kuwa Wapinzani” Waziri Steven Wasira.
Sauti ya Waziri Steven Wasira iko hapa.

No comments:

Post a Comment