Sunday, September 7, 2014

OKWI NI MJANJA SANA, AMFANYA HANS POPPE AWAPIGE BAO LA KISIGINO YANGA SC


Mkali wa sheira?: Emmanuel Okwi (kulia) akiwaonesha ufundi wachezaji wa Gor Mahia siku ya jumamosi uwanja wa Taifa, Simba ikishinda 3-0
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
0712461976
KAMA ubongo wako una uwezo mzuri wa kutunza kumbukumbu, Ijumaa ya Agosti 29 mwaka huu klabu ya Young Africans ilitangaza kumshitaki mchezaji Emmanuel Okwi kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kuwasilisha nakala kwa shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) na shirikisho la soka duniani (FIFA) kwa kuingia mkataba na timu nyingine wakati akiwa bado ana mkataba wa miaka miwili.
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji aliwaambia waandishi wa habari siku hiyo kuwa uongozi wa klabu huyo ulishangazwa na kitendo cha viongozi Simba , wakala  na mchezaji mwenyewe kuingia mkataba wa miezi sita kwa madai kuwa anataka kulinda kiwango chake wakati akiwa na kesi na Yanga.
Manji alisema awali Yanga walipeleka malalamiko TFF na kuwapa nakala CAF na FIFA kuwa Emmanuel Okwi awali alifanya mazungumzo na timu ya Wadi Degla FC ya nchini Misri na kufikia klabu hiyo kutuma ofa ya kutaka kumnunua bila kuwasiliana na uongozi wetu.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com

No comments:

Post a Comment