Tuesday, July 1, 2014

Diamond Kutoa Video Mbili Kwa Mpigo, Na Hili Ni Ombi Lake Kwako

Diamond Platinumz hivi anaendelea kupambana kuupeleka muziki wa Tanzania katika level ya kimataifa na hivi sasa amepanga kuchia video mbili kwa mpigo.
Diamond sasaBila shaka video hizo ni moja aliyofanya na Iyanya Uingereza ambayo amepanga iwe kwa ajili ya mashabiki wa ndani na nje ya nchi na nyingine ya asili ‘MdogoMdogo’ ya Tanzania ambayo mimi naamini pia itafika mbali.
Hata hivyo Diamond ana ombi kwako wewe shabiki wake na ameandika katika ukurasa wake wa Facebook, saidia katika hili tupate tarehe rasmi ya kuzipokea video mbili kwa mpigo.
“Nataka Kudondosha video Mbili kwa Mpigo… tafadhari niambie, lini niziachie…???
[ I wanna drop 2 videos at da same time... Now you tell me, when should I let them out...??]”
Diamond ameweka baadhi ya picha zinazokuwa kwenye video yake akiwa kazini kama muigizaji fulani.
Diamond“Nikikupa Nafasi moja tu ya Kunipa Jina katika Caracter hiyo we ungenipa jina Gani?….. [ If I was to give you a chance to give me a name from that character what would it be...?]”

No comments:

Post a Comment