Sunday, June 22, 2014

Wakenya kuangalia mechi Kombe la dunia nyumbani.

baa
Serikali ya Kenya imewataka wananchi kuangalia mechi za michuano ya kombe la dunia katika maeneo ya majumbani badala ya sehemu za wazi zilizojazana na ambazo hakuna ulinzi.
Ushauri huo umetolewa kufuatia siku mbili za mashambulizi katika mji wa Pwani wa nchi hiyo na kusababisha vifo vya watu 60.
baa2
Mashambulizi hayo yalianzia katika eneo la Mpeketoni ambako mashabiki walikuwa wakiangalia mpira siku ya Jumapili.
Waziri wa usalama wa ndani amesema licha ya kuwa ulinzi umeimarishwa katika maeneo mbalimbali nchini, wamiliki wa baa na migahawa wanatakiwa kuchukua tahadhari zaidi.

No comments:

Post a Comment