Sunday, May 4, 2014

MTAALAM WA NYASI BANDIA KUTOKA FIFA AINGIA NCHINI JANA

Mtaalamu wa nyasi bandia kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Ian McClemen amewasili nchini leo alfajiri (Mei 4 mwaka huu) ambapo atakuwepo kwa siku tatu.

McClemen ameondoka Mei 4 kwenda Bukoba ambapo atakagua Uwanja wa Kaitaba, na kesho Mei 5 atakwenda jijini Mwanza kukagua Uwanja wa Nyamagana.

Viwanja hivyo vinawekwa nyasi bandia kwa ufadhili wa FIFA chini ya mpango wa misaada wa Goal Projects. Baada ya ukaguzi huo, McClemen atatuma ripoti yake FIFA ili shirikisho hilo liweze kuteua mkandarasi wa kufanya kazi hiyo.

Kwa Tanzania viwanja vilivyowekwa nyasi bandia hadi sasa kupitia Goal Project ni Uwanja wa Uhuru uliopo Dar es Salaam, Uwanja wa Karume (Dar es Salaam) na Uwanja wa Gombani uliopo Pemba.

No comments:

Post a Comment