Wednesday, April 23, 2014

Q-CHILA ADAI KUMALIZA UGOMVI WAKE NA CLOUDS FM

Q-Chilla amesema hivi karibuni alienda kukutana na uongozi wa Clouds Media Group kuuomba radhi na kumaliza tofauti zao.

Amesema aliamua kuchukua uamuzi huo kuwa amegundua kuwa kuna wadau wengi aliokuwa amekosana nao kutokana na tabia yake na hivyo angependa kufanya muziki bila kuwa na tofauti na watu.

“Nashukuru Mungu nimeweza kukutana na Ruge Mutahaba, uongozi mzima wa Clouds FM, Joseph Kusaga kukaa chini na kuomba radhi na wao kunikubalia kwa mapenzi yao kwamba ‘huna mchawi, mchawi ni wewe mwenyewe. Ukikaa na sisi meza moja vizuri na kuelewa wapi umekosea unataka kufanya nini sisi tuna nafasi yako kila siku’. Kwahiyo nimeona wakati mwingine naweza nikalaumu watu lakini pia nijiangalie mimi kabla ya kumlamu mtu,” ameiambia Bongo5.

Q-Chilla ameongeza kuwa mashabiki wake wategemee muziki mzuri

No comments:

Post a Comment